Vyombo vya habari vimeripoti taarifa mbalimbali kuhusu
Afya ya Askofu Josephat Gwajima ambae
alikuwa amelazwa katika Hospitali ya TMJ toka siku ya Jumamosi baada ya
kuanguka wakati akihojiwa na Polisi Makao Makuu DAR.
“Hali ya Afya yangu inaimarika
naendelea vizuri sasa.. nasema viongozi wa dini lazima wawe wakweli jambo
linaloamuliwa na viongozi wa dini lazima kiongozi wa dini aheshimu na amentain
kile kilichokuwa kimesemwa na maaskofu” –Askofu Gwajima.
Daktari aliyekuwa akimhudumia Askofu huyo katika
hospitali TMJ amesema
kuwa Afya ya mgonjwa wake inaendelea vizuri; “Ni kweli kwamba tulikuwa tumemlaza MchungajiJosephat Gwajima katika Hosptitali yetu kuanzia siku ya
Ijumaa ya tarehe 27.. tulimlaza ICU na amekaa kule kule ICU kuanzia siku ya
Ijumaa hadi Jumatatu alipopata nafuu kidogo tukamuondoa ICU, tukampeleka general ward ambapo
ameendelea kutibiwa kutoka ile jana hadi Jumatatu mpaka leo Jumanne, tukaona
hali yake ime improve kwa kiasi kikubwa na tukaona pamoja kwamba sio kwa
asilimia mia moja, lakini anaweza kuruhusiwa kwenda nyumbani na anaweza
kuendelea na matibabu akiwa nje.“–Dr.Fotrunatus Mazigo.
Kuhusu
kuwa na walinzi Hospitalini hapo daktari amesema ni kweli alikuwa na walinzi.
Post a Comment