Anaitwa Jennifer Kyaka, ila wengi wamezoea kumuita ODAMA,
jina ambalo liliibuka kwenye movie ya Odama aliyoigiza, ambapo yeye alicheza
kama mhusika mkuu. Alizaliwa mnamo mwaka 1983 jijini Mwanza katika Hospital ya
Bugando.
Safari yake ya sanaa ilianza mnamo mwaka 2006, na movie yake ya kwanza kuigiza ilikuwa inaitwa SHUMILETA, Movie iliyoandaliwa na producer na director maarufu nchini, Mussa Banzi, watu wengi walianza kumfahamu kwenye movie hiyo ya kutisha aliyocheza kama Monte.
Movie ya Shumileta ilimfungulia milango, ambapo mrembo huyo asiye na makuu alianza kuonekana kwenye movies kadhaa ikiwemo, ODAMA, BEYONCE, VERONICA, BROKEN HEART na nyinginezo.
Jina lake likazidi kukua, watu wakamtambua zaidi kutokana na kipaji na uhodari wake wa kuigiza kwa hisia za hali ya juu na kuuvaa uhusika vilivyo ,movie kama ODAMA na VERONICA zinatajwa kuwa miongoni mwa movie zilizomuweka muigizaji huyo kwenye ramani nzuri kwenye sanaa , haswa kutokana na uhalisia alioubeba kwenye movies hizo.
Baadae aliamua kuandaa movies zake mwenyewe kupitia kampuni yake ya J-FILM FOR LIFE, ambapo ndani ya kampuni hiyo alitengeneza movies zisizopungua 30, movies kama LIFE 4 LIFE, LOREEN, CHOCOLATE, RUDE, PAIN KILLER, WHITCH DOCTOR, INSIDE, JICHO LANGU na JADA ambayo mpaka sasa ivi inafanya vizuri sokoni kwa mauzo.
Muigizaji huyo ambaye pia ni mama wa mtoto mmoja, anatajwa kuwa ni miongoni mwa producers wenye mpunga mrefu apa nchini, japokuwa mwenyewe hataki kujionyesha kuwa anazo. Pia anatajwa kujenga nyumba na kumiliki magari kadhaa pamoja na kampuni na kumiliki biashara, ni moja ya mafanikio anayojivunia muigizaji huyo mwenye uzuri wa asili na mvuto wa aina yake.

Post a Comment