Taasisi
ya dini ya Kiislam imeitaka serikali kuwakamata maaskofu na wachungaji
ambao inadai wametoa matamko ya kichochezi na endapo serikali itashindwa
kuwakamata, basi jumuiya hiyo itawahamasisha waamini wa dini ya kiislam popote
walipo kuipigia kura ya Hapana Katiba inayopendekezwa na Bunge
Maalum la Katiba.
Kauli
ya taasisi hiyo yenye misimamo mikali inatokana na Tamko lililotolewa na
muunganiko wa jumuiya ya Kikristo,ikiwemo Baraza la Maaskofu katoliki
(TEC),Jumuiya ya Kikristo Tanzania(CCT) na Baraza la Makanisa la
kipentekoste(CPCT) ambao wote kwa pamoja waliwataka waumini wa dini ya
kikristo nchini kuipigia kura ya Hapana katiba inayopendekezwa
kutokana na serikali kuruhusu mahakama ya Kadhi kisheria.
Akitoa
tamko la Taasisi ya Dini ya Kiislam ambalo ni muunganiko wa taasisi za
dini hiyo zaidi ya 11 hapa nchini,Naibu Katibu Mkuu wa Taasisi hiyo Sheikh
Rajab Katimba wakati wa Mkutano na Vyombo mbalimbali vya
habari jana Jijini Dar es Salaam, aliitaka serikali
kuwachukulia hatua maaskofu hao kwa madai ya kufanya uchochezi.
“Serikali
iwachukulie hatua za kisheri maaskofu na wachungaji kwa kutoa matamko
yakichochezi yaliyokusudia kuumiza hisia ya kidini kwa waislam kinyume cha
sheria ya kanuni ya Adhabu sura ya 16.
"Tunataka Maaskofu hao wakamatwe,wafikishwe mahakamani na dhamana izuiliwe kama inavyofanya kwa masheikh pindi wanapotoa kauli zinazopingana na mtazamo wa serikali, lasivyo hatutaipigia kura ya Ndiyo katiba iliyopendekezwa”alisema Seikh Katimba.
"Tunataka Maaskofu hao wakamatwe,wafikishwe mahakamani na dhamana izuiliwe kama inavyofanya kwa masheikh pindi wanapotoa kauli zinazopingana na mtazamo wa serikali, lasivyo hatutaipigia kura ya Ndiyo katiba iliyopendekezwa”alisema Seikh Katimba.
Aidha,
Sheikh Katimba aliitaka Serikali kuendelea na Mchakato wa uundwaji
mahakama ya kadhi kwa kufuata maoni yaliyotolewa mbele ya kamati ya sheria na
utawala wa bunge kwa kuzingatia mambo muhimu mawili.
Mosi: Serikali iache njama na hila
za kuigeuza mahakama ya Kadhi inayohitajika kuwa miliki ya taasisi ya BAKWATA
na MUFTI wa BAKWATA.
“Endapo
serikali itaendelea na kuwasilisha muswaada wa Mahakama ya Kadhi unaoipa
mamlaka Bakwata kuunda, kusimamia,kuteua makadhi nakadhalika kinyume na maoni
ya Waislam wengi itakuwa imethibitisha kuwa serikali haikuwa na nia ya kweli ya
kuunda na kuanzisha mahakama ya Kadhi” alisema
Sheikh Katimba.
Pili: Serikali igharamie mahakama
hiyo kama inavyogharimia uendeshaji wa mashauri yaliyopo kwenye mahakama za
kawaida yanayohusu sheria za kiislam ambayo mara nyingi yanaamuliwa kwa makosa.
“Na
pia mahakama hiyo igharamiwe na serikali kama inavyogaramia huduma
za makanisa chini ya mkataba maarufu uitwao memorandum of understanding (MOU) ,
mkataba ambao haukuwahusisha wala kutaka ridhaa ya waislam” alisema sheikh
huyo
Post a Comment