ABIRIA 13 wakiwemo watatu wa familia moja wamefariki dunia
mkoani Singida leo, baada ya gariwalilokuwa wakisafiria aina ya Noah T.730 BUK,
kugongwa na Lori aina ya Scania.Ajali hiyo ya kusikitisha imetokea leo saa 1.32
asubuhi katika barabara kuu ya Singida-Dodoma eneo la kijiji cha Isuna tarafa
ya Ikungi wilaya ya Ikungi mkoani Singida.
Kamanda wa polisi mkoa wa Singida, SACP , Geofrey Kamwela, amesema gari hilo aina ya Noah lilikuwa likitokea Itigi wilaya ya Manyoni nalilikuwa na safari ya kuja Singida mjini.
Amesema hadi sasa miili ya abiria 10 wamekwisha tambuliwa na ndugu zao na miili ya abiria watatu, bado haijatambuliwa na miili yote bado imehifadhiwa kwenye chumba cha kuhifadhia maiti cha hospitali ya mkoa mjini Singida.

Post a Comment