Haya hii ya leo ngoja niwatobolee siri kidogo tu
kwenye upande wa mapenzi. unajua wanawake bwana tupo kama mayai ukiyaminya
kidogo tu huwa yanapasuka.. sasa wengi wanaume huwa wanabaki kuropoa “wanawake
hawaeleweki” WANATAKA TUWEJE? Mwanamke huwa anapenda sana kuambiwa ukweli japo
wengi wanadai eti bila kudanganywa hatuingiliki, Wanawake wengi hupenda kuspend
muda wake zaidi na wake mpenziuliko na marafiki zake. Mwanamke hupenda mwanaume
anaejali zaidi kuliko mbabaishaji “sasa wewe jifanye gogo tuone kama utapata
mrembo” Jeuri ufanyiapo mwanamke dhahir huwa unamvunja moyo na hukushusha
thamani yako pindi umfanyiayo yakawa yale yanayo mdharaulisha zaidi Mthamini
mpenzi wako hata ukiwa na watu wengi, onyesha unajali kuwa nae karibu, hujiona
wa pekee Mwanamke hupenda kusikilizwa japokuwa wanaume hujifanya vichwa na
kutuona hatuna la kuongea lakini sio kweli ni fikra zenu tu. Msikilize mpenzi
wako uone kama na wewehatokusikiliza Mwanamke huthamini sana msg za mpenzi wake
kuliko simu apigiwayo na mwenza wake, maana kuona faraja zaidi pindi asomapo
msg hizo zaidi ya kupoteza muda kusubiri apigiwe au akupigie. Msifie mkeo ama
mchumba wako pindi apendezapo na kumpa faraja pindi aumizwapo. Msikilize
mchumba wako na usitumie lugha ya ukali akuombapo ushauri bali jaribu
kuchunguza zaidi nini atakacho kwako. Kila lililo dogo usilikuze bali lipe
nafasi yake katika kutoa kipingamizi ama makubaliano.lasivyo utasababisha
kutokujiamini.Onyesha unajali Mkumbuke kila wakati hata mara2 kwa siku Punguza
jeuri na kauli chafu ukifananya kati ya hayo hutopata misukosuko mingi na
kumbuka kujishusha endapo ufanyapo kosa na acha kutumia mabavu zaidi kuliko
upole. haya jamani ni hayo tu labda utaona umuhimu wa mwenza wako zaidi ya
kuliko kutoa lawama juu yake, wapendwa kama hamtojali kama kuna ambayo wakina
kaka nao wanataka kutoa kero zao uwanja wenu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment