Miongoni
mwa taarifa zilizochukua Headlines katika taarifa ya Habari ya kituo cha ITV ni
hii ya Kiongozi wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Askofu Josephat Gwajima ambae amefika kituo kikuu cha Polisi
Dar kwa ajili mahojiano na Jeshi la Polisi kwa madai ya kutoa kauli yenye
maneno makali kwa kiongozi wa Kanisa Katoliki, Askofu Kardinali Pengo.
Askofu Gwajima amesema maneno aliyoyatoa ni ya
kumkemea kiongozi mwenzake wa kiroho kwa madai ya kukiuka msimamo wa viongozi
wenzie wa dini wa kukataa Mahakama ya Kadhi.
“Baraza la Maaskofu Tanzania waliamua kwa pamoja na
wakasaini waraka kwa pamoja, kwamba hawataki Mahakama ya Kadhi… lakini
tukashangaa mwenzetu Askofu
Pengoaliyesaini na yeye anageuka sasa tukajiuliza kwa nini anageuka?
mimi kama kiongozi wa kiroho nikaona nimkemee.. lakini nimeitwa na Polisi sasa
najiuliza niliyemkemea ni Polisi au nilimkemea nani?“ –Askofu Gwajima.
Hivi karibuni katika mitandao ya kijamii kumezagaa picha za
video zenye maneno ya kashfa kwenda kwa kiongozi wa Kanisa Katoliki Askofu Kardinali Pengo jambo lililofanya jeshi la Polisi
kumtaka afike kituoni kikuu cha Polisi kwa mahojiano.
Post a Comment