‘SARAKASI’ za Mkutano wa 19 wa Bunge la 10 zitaanza leo mjini Dodoma na imeelezwa kuwa ni maalum kwa ajili ya kushughulikia miswada ya sheria ikiwemo Sheria ya Makosa ya Mtandao (The Computer and Cyber Crimes Bill, 2015) na ya vyombo vya habari ambazo tayari zimetinga bungeni.
Kwa mujibu wa taarifa ya Idara ya Habari, Elimu kwa Umma
na Uhusiano wa Kimataifa ya Bunge, jumla ya miswada sita itawasilishwa bungeni
kwa Hati ya Dharura na inakusudiwa kupitishwa katika hatua zake zote.
Pamoja na Muswada wa Sheria ya
Makosa ya Mtandao, mingine ni Muswada wa Sheria ya Kupata Habari wa Mwaka 2015
(The Access to Information Bill, 2015), Muswada wa Sheria ya Vyombo vya Habari
wa Mwaka 2015 (The Media Services Bill, 2015) na Muswada wa Sheria ya
Marekebisho ya Sheria ya Ushindani wa Mwaka 2015 (The Fair Competition
Amendment Bill, 2015).
Miswada mingine ni Muswada
wa Sheria ya Miamala ya Kielektroniki wa Mwaka 2015 (The Electronic Transaction
Bill, 2015) na Muswada wa Sheria ya Gesi Asilia wa Mwaka 2015 (The
Natural Gas Bill, 2015).
Kuja kwa miswada ya habari
kunaweza kuwa ‘ukombozi’ kwa wana habari kwani wamekuwa wakiilalamikia
serikali, baadhi yao wakidai kuwa sheria zilizopo zinakandamiza na kuwanyima
kupata habari. Vikao hivyo vya bunge vitamalizika Aprili Mosi, mwaka huu.
Post a Comment