Staa wa Bongo Movies na Bongo Fleva,
Zuwena Mohamed ‘Shilole’, juzikati alijikuta akilewa chakali kiasi cha
kushindwa kupanda boti iliyokuwa imeandaliwa maalum kwa ajili ya kwenda
kusherehekea tukio la kukatwa keki katika kumbukumbu ya siku ya kuzaliwa ya
msanii mwenzake, Estelina Sanga ‘Linah’, iliyofanyika Slipway, Masaki jijini
Dar.
Shilole alikuwa amealikwa kwenye
sherehe hiyo iliyoanza kurindima jioni ya saa 10 ndani ya Ukumbi wa Paparazi,
ambapo waalikwa walianza kupata mapochopocho zikiwemo pombe na baadaye kutakiwa
kupanda boti ili kwenda kumalizia sherehe katikati ya maji kwa kukata keki.
Kutokana na kubugia kiburudisho
kupita kiasi, Shilole alishindwa kupanda boti iliyokuwa imeegeshwa pembeni mwa
bahari na hivyo kumpa kazi ya ziada mchumba wake Nuh Mziwanda aliyelazimika
kumrudisha garini ili warejee nyumbani.
“Kusema kweli mimi hata sielewi
nilishindwaje kupanda boti, network ilikata, nilishangaa tu kujikuta nipo
kwenye bethidei ya Menina Mikocheni, nafikiri kilichotokea muulize baby wangu
Nuh Mziwanda,” alisema Shilole baada ya kuulizwa kuhusu ‘kuzimika’ kwake.
Nuh Mziwanda alikiri kuwa mpenzi
wake alipoteza fahamu, kiasi cha kumlazimisha yeye kumbeba na kumrudisha tena
klabu ya Paparazi ambako alipatiwa maji baridi kwa wingi huku akipigwa na
kiyoyozi cha nguvu kabla ya kwenda kwenye shughuli ya Menina.
-GPL
Post a Comment