Baada ya uvumi kusambaa kuwa mchekeshaji wa kundi la Orijino
Komedi Venguamefariki na
baadae kaka yake alikanusha uvumi huo, kiongozi wa kundi hilo Sekioni David amesema
wamepata usumbufu mkubwa juu ya uvumi huo na wao kama kundi wameamua kuchukua
hatua zaidi ili kukomesha tabia hiyo kwa kuwa sio mara ya kwanza,
wamepata ushauri kutoka TCRA ambao wamewashauri kuchukua hatua ili kuweza kujua
chanzo cha uvumi huo na kuchukua hatua zaidi kwa wahusika na muda sio
mrefu mhusika atajulikana
Kuhusu Afya ya Vengu amesema ni mzima ila kutokana na
ushauri wa daktari anatakiwa awe kwenye utulivu ambao unamfanya awe nje ya
kundi lakini yeye bado ni mfanyakazi na anaendelea kulipwa kama kawaida.
Post a Comment