Mpaka
April hii ya 2015 kwenye muziki wa dance Tanzania hii haikosi kuwa kwenye stori
2 za juu nina uhakika, tunajua Ali Choki ndio alikua anaimiliki band ya Extra
Bongo na baadae aliwachukua watu kama Banza Stone na Super Nyamwela lakini
April 8 2015 headlines zimegeuka.
Mkurugenzi Asha Baraka ameongea kwenye Exclusive interview na Millard Ayo baada
yaAli Choki na dancer Super Nyamwela kutangazwa
kurudi Twanga Pepeta >>>
‘Kwanza tulikua na kutokuelewana
nafikiri ni kibiashara kati yangu mimi na Ali Choki lakini baadae watu wazima
wakakaa wakaona ili kukuza tasnia wakatuweka chini Global Publishers na wakatuweka sawa‘
‘Kilichotokea
baada ya hapo Ali Choki alikwenda Japan kwenye safari zake na akiwa huko
akasikia huku nyumbani Wanamuziki wake wametawanyika naona akaona ni vigumu
tena kuanzisha Band na kujipanga upya kwa hiyo akaamua kurudi kwenye Band yake
ya Twanga Pepeta iliyomkuza na kumfanya kuwa Choki’ – Asha
Baraka.
Post a Comment