Staa mrembo wa
Bongo Movies na Bongo Fleva, Shilole ‘Shishi Bybee’ amewataka watu wamuache
afanye kile anachokitaka kwenye maisha yake na sio kumpagia aishi vipi.
Shishi
Bybee aliyasema hayo mara baada ya baadhi ya watu kumshambulia kwa maneno baada
ya kuweka picha picha akiwa yupo kwenye bwawa la kuogelea.
“Yaani watu mnapenda kunipa raha sana mimi mwenywe
nimejikubali na mimi nipo swimming mlitaka nivae dela??? Nioge nalo kwa hiyo
tunapangiana na maisha ya nyumban pia lol! Kila mtu na life yake naombeni
mniache nifanye yangu” Shishi
alisema.
Baadhi
ya watu walionyeshwa kukelwa na picha hizo (hapo juu) za Shilole wakidai
kuwa zinamdhalilisha kama mwanamke kwani sehemu kubwa ya mapaja yake yapo wazi.
Post a Comment