Wanaume wanapendelea wanawake wenya makalio
makubwa
Je wajua kwanini wanaume wanawapenda wanawake
waliojaliwa na makalio makubwa ?
Katika majarida mengi umewaona wanaume
wakikodolea macho picha za wanawake wenye makalio makubwa iwe ni kim
Kardashian, Jenipher Lopez Nicki Minaj na Vera Sidika kutoka Kenya .
Sasa basi Utafiti umedhibitisha kuwa ni kweli
wanaume wanapenda wanawake waliojaaliwa sehemu ya nyuma.
Kulingana na utafiti wa chuo kikuu Bilkent ,
chuo kikuu cha Texas, na chuo kikuu cha American University kilichoko mjini
Beirut
Wanaume wanakisia kuwa mwanamke mwenye makalio
makubwa anaweza kufanya kazi kwa bidii zaidi ya mwanamke ambaye hana makalio
makubwa.
Hata hivyo kinachowavutia wanaume si makalio
haswa bali ni kupinda kwa uti wa mgongo unaosababisha tako kuonekana zaidi.
Utafiti huo unasema kuwa upinde wa 45.5 ndio
unaovutia wanaume zaidi.
Wanaume walioneshwa picha za makalio ya
wanawake wengi na asilimia kubwa iliwapendelea wanawake wenye makalio
yaliyopinda kwa kiwango cha 45.5
Aidha zaidi ya asilimia 30% walisema
wangalimchukua mwanamke mwenye makalio makubwa zaidi ya yule waliye naye sasa.
Kwa mujibu wa utafiti huo katika miaka ya
awali mwanamke aliyeonekana kuwa na makalio makubwa alipendelewa kutokana na
uwezo wake wa kubeba mizigo mgongoni.
Isitoshe mwanamke kama huyo aliwavutia wanaume
wengi na hivyo kuwa na uwezo wa kuzaa watoto wengi.
Aidha mwanamke mwenye
makalio makubwa angeweza kustahili uzito wa mtoto aliyebebwa tumboni na hata
kustahilimi makali ya uzazi kuliko wale wenye makalio wastani
Post a Comment