Ikiwa
mwanamke anampenda sana mumewe basi mwanaume atakuwa na matatizo ya
kianasaanasa, hata kwa mwanaume anayempenda mkewe basi sehemu kubwa mkewe anakuwa
ana shida.
Mpenzi msomaji, asikudanganye mtu
kupendwa kuna raha yake, tena mno kuliko kupenda. Unapopendwa una nafasi kubwa
ya kufanya chochote unachotaka kama vile kudeka, kujishebedua, kuzira,
kulazimisha kisichokubalika na kukubalika n.k.
Kwa
wale wanawake wajanja hii ndiyo huwa sehemu ya kutusua kwa maana ya kufanya
vitu vya maendeleo akijua kuna jamaa kamshika kwa sababu kazimika basi anatumia
mwanya huo, kuvuta mkwanja na kuomba kufunguliwa miradi kadha wa kadha ili hata
kama mapenzi yakiisha yeye anakuwa na faida.
Ila kama wewe ndiyo unapenda, ujue
kabisa huna nafasi hiyo zaidi ya kuumizwa na mwenzi wako kila kukicha, wewe ni
mtu wa majonzi, majuto, kilio na maumivu ya moyo kwani kuna muda anaweza
akakufanyia lolote baya analotaka na wewe usikasirike zaidi ya kumbembeleza na
wakati mwingine kujitwisha gunia la misumari kwa kujifanya wewe ndiye mwenye
makosa ilimradi tu usimuudhi mwenzi wako. Anaweza akaamua kutojibu meseji au
kutopokea simu yako, akijua wazi anakumudu na huna chakuzungumza juu yake. Hata
kama mkikutana na kumuuliza, atakujibu anavyotaka akijua ameushikilia moyo
wako.
Mara nyingi wapenzi wanaopata nafasi
ya kupendwa na wenza wao wamekuwa wakitumia silaha hiyo vibaya, ikiwemo
kuwaumiza wapenzi wao kwa tabia zao chafu kama umalaya, matusi, kejeli, dharau,
masimango, kununa, kulazimisha kununuliwa kitu anachokitaka au apelekwe kiwanja
cha starehe, kula anachotaka hata kama mfuko wa mpenzi wake haujitoshelezi.
Kinachotumika hapo ni nguvu ya penzi, nguvu ya yeye kupendwa na mtu huyo.
Angalizo; kama utatumia nafasi ya
kupendwa vibaya utakuja kuachwa ukiwa katika wakati mgumu, kwani
inaonesha kuwa watu wenye kupenda na kutendwa ni wavumilivu sana ila wenye
uamuzi mgumu na mzito wanapofika mwisho, na hata wakiamua uamuzi wao huwa hauhitaji
ushauri wa ndugu, marafiki au viongozi wa dini. Huwa wanasema ‘potelea mbali,
haikuwa riziki yangu’. Tumia vizuri nafasi hiyo ya kupendwa na siyo kumkomoa
mwenzi wako. Tukutane wiki ijayo kwa mada nyingine tamu.
Post a Comment