Timu ya Simba ya Dar es Salaam huenda ikaachana na
wachezaji wageni kutoka Uganda iwapo tu mawazo ya kocha mkuu wa klabu hiyo
kutoka Serbia, Goran Kopunovic yatatekelezwa na uongozi wa timu hiyo.
Kocha
huyo amesema haoni kama wachezaji hao wanafaa kuichezea Simba ila asingependa
kuongea zaidi maada hata yeye mkataba wake umekwisha, hajui kama atabaki au la.
Habari
zinasema kutoks vyombo vya habari zinasema kuwa Simba wameachana na mfungaji
bora wa zamani wa Ligi Kuu ya Kenya, Danny Sserunkuma baada ya makubaliano ya
pande zote mbili.
Habari
zinasema kuwa mshambuliaji huyo raia wa Uganda aliandika katika ukurasa wake wa
twitter akisema kuwa amefikia maamuzi ya kusitisha mkataba na hata ichezea
Simba katika msimu ujao.Sserunkuma alisajiliwa na Simba mwezi Desemba mwaka
jana akipewa mkataba wa miezi 12 ambayo ilikuwa inatarajiwa kumalizika mwaka
huu.
Hadi
anaondoka Simba SC, Sserunkuma aliyetokea Gor Mahia ya Kenya alikuwa amecheza
mechi 17 na kuifungia mabao matano katika mashindano yote ikiwemo ligi kuu
iliyomalizika hivi karibuni huku Yanga ikitwaa ubingwa.
Habari
kutoka klabu ya Simba, ambayo imemaliza nafasi ya tatu katika ligi iliyoisha ni
kwamba kocha mkuu, Goran Kopunovic amesema anahitaji kubaki na wachezaji wawili
tu wa kigeni katika kikosi cha msimu uliopita na kwa tafsiri hiyo, wachezaji
wengine, Simon Sserunkuma na Joseph Owino, wote Waganda, nao huenda wakaondoka
muda wowote.
Wachezaji
wengine wa kigeni kikosini Simba SC ni Waganda pia, Juuko Murushid na Emmanuel
Okwi, ambao huenda wakasalia katika kikosi hiko kwa ajili ya msimu ujao.
Post a Comment