Kiungo mshambuliaji wa timu ya
taifa ya Tanzania Mrisho Khalfan Ngassa amesaini mkataba wa miaka minne
kuichezea timu ya Freestate Stars inayoshiriki ligi kuu ya soka nchini Afrika
Kusini maarufu kama PSL .
Ngassa amesaini mkataba huo siku
chache baada ya kuisaidia klabu yake aliyoitumikia kwa muda mrefu ya Dar es
salaam Young Africans kutwaa ubingwa wa ligi kuu ya soka Tanzania bara .
Ngassa amekuwa akisakwa na timu hii
ya Afrika Kusini kwa muda mrefu ambapo iliwahi kutuma ofa ya kumsajili tangu
msimu uliopita lakini Yanga waliikataa ofa hiyo kwa sababu ilikuwa ndogo .
Mrisho Ngassa amekuwa akisakwa na
timu nyingi za nje ambazo zimevutiwa na uwezo wake na kwa nyakati tofauti ofa
kadhaa zimewahi kutumwa kwenye klabu ya Yanga kwa ajili yake .
Klabu za Al Mareikh ya Sudan pamoja
na Seattle Sounders ya Marekani zimewahi kumtaka Ngassa na Sounders wamewahi
kumpa nafasi ya kufanya majaribio katika mchezo dhidi ya Manchester United
miaka kadhaa iliyopita .
Ngassa huenda akaungana na mchezaji
mwenzie wa Yanga na timu ya taifa Simon Msuva ambaye hivi karibuni alifanya
majaribio na klabu ya Bidvest Wits na kama timu hiyo ikiridhishwa na kiwango
chake huenda akasaini mkataba .
Post a Comment